Mchengerwa Aipongeza SPANISH TILES Kwa Ujenzi Jengo la Saratani

0


Na WAF, Arusha

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa pongezi kwa taasisi ya Spanis Tiles iliyofanikisha Ujenzi wa Jengo la Utoaji wa huduma za Saratani kwa mkoa wa Arusha na Mikoa ya jirani.

Waziri Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Januari 26, 2026 alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha huduma za wagonjwa wa saratani chini ya ufadhili wa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.

Katika uwekaji wa jengo hilo Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe kuwa ndani ya wiki mbili vifaa viwe vimefikishwa na Watanzania waanze kupata matibabu ya saratani katika kituo hicho kipya.

Aidha, ameishukuru kampuni ya Spanish tiles chini ya Mkurugenzi wake Bw. Bobby Chadha kwa mchango wake mkubwa wa ujenzi huo na ametoa rai kwa wafanyabiashara wengine kuja kuwekeza katika sekta ya Afya ili kupunguza gharama za matibabu na kuendelea kuokoa maisha ya wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa Spanish Tiles  Bw. Bobby Chadh akitoa salam za kampuni ameishuru Serikali kwa jinsi inavyoshirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwahudumia wananchi. 

Bw. Bobby amesema wameitikia wito wa Mhe. Rais wakutaka kuzidi kuboresha huduma za afya kwenye mkoa huo kutokana na mkoa huo kuwa na Watalii wengi.

Aidha Bw. Bobby ameridhia ombi la Mhe. Mchengerwa ambapo alimwambia mwekezaji huyo, Serikali ipo tayari kumuonesha Mwekezaji maeneo mengine yenye uhitaji ili kuweza kusogeza huduma hiyo kwenye maeneo husika.


Kukamilika kwa jengo hilo, itaokoa muda na gharama za uchumi wa wananchi badala ya kusafiri hadi Ocean Road au maeneo mengine ya ndani na nje ya nchi, sasa huduma hizo zinapatikana mkoani hapo.








Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top