Serikali Yatoa Mwelekeo Mpya Katika Uwekezaji Viwanda vya Bidhaa za Afya Nchini

0


Na WaF, Dar es Salaam

Serikali imetangaza rasmi mwelekeo mpya wa kimkakati wa kuharakisha uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini ikiwa ni lengo la kuimarisha usalama wa afya wa nchi, kupunguza utegemezi wa dawa, na kuliweka taifa kwenye ramani ya uzalishaji wa dawa barani Afrika na Duniani.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Desemba 23, 2025 katika kikao cha wazalishaji wa dawa na bidhaa za afya pamoja na uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji mchakato wa uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam.

“Ujenzi wa viwanda vya dawa si mpango wa majaribio bali ni uamuzi wa kimkakati uliokwisha amuliwa na Serikali, usalama wa afya wa Taifa hauwezi kujengwa kwa kutegemea uagizaji wa dawa pekee, bali unahitaji uzalishaji wa ndani unaokidhi viwango vya kimataifa” amesema Waziri Mchengerwa.

Amebainisha kuwa Serikali imeanzisha mfumo maalum wa uharakishaji wa uwekezaji nchini kupitia Green-Lane Approval System, unaotekelezwa chini ya programu ya kuharakisha uwekezaji wa bidhaa za afya nchini ’Pharmaceutical Investment Acceleration Programme’ pamoja na kuunda kikosi kazi maalumu Pharmaceutical Investment Acceleration Taskforce (PIAT) kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ya kuboresha uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini.

“Tumeondoa urasimu wa maamuzi ya mizunguko mirefu, mwekezaji mwenye nia ya dhati atapata majibu ya haraka, ya wazi na yanayotabirika,” amesisitiza Waziri Mchengerwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wamiliki wa Viwanda vya Dawa nchini Bw. Bashir Haroon amesema kuwa wapo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ili kufikia ndoto za uzalishaji wa ndani kikamilifu wa bidhaa za afya na Wananchi waweze kunufaika zaidi na upatikanaji wa uhakika wa dawa nchini kwa gharama nafuu.

Ameopongeza Serikali kwa hatua nzuri ya kufungua zaidi milango kwa wawekezaji wa viwanda vya dawa nchini na kuiomba Serikali kufanyia kazi kwa haraka changamoto wanazo kutana nazo wazalishaji wa bidhaa za afya nchini ili waweze kupanua wigo wa uzalishaji wa bidhaa za afya nchini.

Chanzo: wizara ya afya








Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top