Dkt. Nchimbi Mgeni Rasmi Uwekaji wa Jiwe la Msingi Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tawi la Bukoba

0



 Na Angela Sebastian 

Bukoba : Makamu wa Rais Dk.Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe la msingi wa tawi la chuo kikuu cha Dar Es Salaam tawi la Bukoba kinachojengwa  kata ya Itahwa Bukoba vijijini Mkoani Kagera. 

Hayo yameelezwa mkuu wa mkoa huo Hajati Fatma Mwassa wakati akiongea na waandishi wa habari  ofisini kwake ambapo amesema uzinduzi huo utafanyika Desemba 15 mwaka huu ambapo pia uzinduzi huo utaudhuliwa na Rais mstaafu wa hawamu ya nne Dk.Jakaya Mlisho Kikwete ambaye ni mkuu wa chuo hicho.

Amezitaja fursa za uwepo wa chuo kikuu hicho kuwa ni kujipanga zaidi kwani mji wa Bukoba unaenda kukua zaidi,kuongeza ajira,kukuzakipato cha wananchi maana watazalisha bidhaa na mahitaji ya nyumba za kupanga za kupanga kwa ajili ya wageni yataongezeka.

Kwa upande wake Naibu mratibu wa mradi wa chuo hicho Profesa  Liberato Haule amesema kuwa chuo hicho kitakapokammilika ,kitakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi  800 na awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/207 chuo kitapokea wanafunzi 660 awamu ya kwanza  huku matarajio yao ifikapo 2030 wafikie wanafunzi 1600.

Amesema chuo kitatoa masomo ya biashara na tehama pia kutakuwa na kituo cha kutoa ushauri kwa wafanyabiashara.






Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top