Madaktari Bingwa wa Mama Samia Waanza Kambi ya Siku Tano Mkoani Kagera

0


 Angela Sebastian

Bukoba : Madaktari bingwa na ubingwa bobezi na wauguzi wabobezi wapatao 48 wa mama Samia Mentorship wameanza kambi ya siku tano ya utoajia huduma za kibingwa kwa wananchi wa Halmashauri nane za mkoa wa Kagera .

Akiongea na waandishi wa habari  jana mjini Bukoba katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo,kiongozi wa timu hiyo kutoka wizara ya Afya Dk. Patrick Kushoka ambaye pia ni bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi  amesema kuwa, wapo madaktari wa kada mbalimbali wakiwemo wale wa magonjwa ya wanawake na uzazi pia ganzi na usingizi  ambapo licha ya utoaji huduma kwa wananchi watawajengea uwezo wataalam wa ndani ya halmashauri hizo.

Alisema kuwa madaktari hao 48 watakuwa mkoani Kagera kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakazi wote wa Mkoa wa Kagera na maeneo jirani na kuwa hata huduma zaupasuaji pia  zitafanyika katika vituo husika.

“Tutakuwa kwenye Halmashauri zote nane za mkoa huo ambapo tunatarajia wananchi wengi kwani wapo madaktari bingwa na wauguzi wabobezi ambao watahudumia magonjwa ya kinywa na meno,upasuaji,magonjwa ya mkojo kwa akina baba,magonjwa ya watoto,magonjwa ya ndani kama vile kisukari na shinikizo la damu na magonjwa ya akina mama ambayo hujulikana kama magonjwa ya wanawake na uzazi”amesema

Madaktari hao ambao kabla ya kuwatanywa kwenye halmashauri wamefika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kujitambulisha wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata huduma 

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera DK. Samuel Laizer alisema kuwa hii ni mara ya nne madaktari kufika na kutoa huduma na hivyo kwa awamu zile tatu zilizopita zaidi ya wananchi elfu sita waliweza kupata huduma.

Alisema uwepo wa huduma hii itasaidia wananchi wa Kagera kupunguza  adha ya kufuata huduma mbali.




Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top