Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Afya Nyabiyonza Wilaya ya Karagwe Wafikia Asilimia 98

0


 Na. Angela Sebastian 

Karagwe: Wananchi 12,325 wa tarafa za Nyabiyonza na Nyakakika Wilayani Karagwe mkoani Kagera wanatarajiwa kupata huduma bora katika kituo cha Afya Nyabiyonza ambacho kimefikia asilimia  98 ya ujenzi.

Agnes Mwaifuge ni mganga mkuu wa Wilaya ya Karagwe wakati akisoma taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi amesema mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 640.1 na utakapokamilika utaboresha huduma stahiki  kwa wananchi ikwemo akina mama wajawazito na watoto wachanga ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Amesema ujenzi wa kituo cha Afya Nyabiyonza ulianza Oktoba 25,2024 na unatarajiwa kukamilika Septemba 25 mwaka huu ambapo umefikia asilimia 98 na yapo majengo matano ikiwemo jengo la upasuaji,wagonjwa wa nje,wodi ya wazazi,maabara jengo la kufulia na kichomea taka .

Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi ametembelea na kuweka jiwe la msingi Katika mradi huo na kuridishwa na maendeleo ya utekelezwaji wake ambapo amewaomba wanachi kutoa ushirikiano kwa madaktari watakaoletwa hapo kwasababu ni watu muhimu pia kazi yao ni ngumu.

Ameeleza kuwa madaktari wanatibu watu wa aina mbalimbali ambao hata hawajui wamezaliwa au wametokea wapi lakini wao wanaendelea kutoa huduma kwa umakini wa hali ya juu.

Aidha amewashauri wananchi kuendelea kupambana na ugonjwa wa maralia chini ya kauli mbiu isemayo ziro malaria inaanza na mimi,wewe na sisi sote.

Levina Luchumis ni mwananchi wa Nyabiyonza anasema Zahanati hiyo inaenda kuboresha huduma za Afya kwa wananchi hasa akina mama wanapokwenda kijifungua walikuwa wakiteseka sana,mpaka waende hospitali ya  Nyakahanga iliyopo kilometa 17.

Kwa upande wa mkuu wa Wilaya ya Karagwe Kalanga Laizer akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaitun Msofe

amesema Mwenge utakagua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya  zaidi ya shil billion 3.5.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top