Na Angela Sebastian
Bukoba : Mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini Mhandisi Johnston Mutasingwa ametaja sababu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo ambapo ni kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati aliyotekeleza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Mutasingwa amesema katika jimbo la Bukoba mjini Dk.Samia ametekeleza miradi mbalimbali katika idara ya elimu,Afya,barabara,maji,standi kuu ya mabasi sambamba na soko kuu la Bukoba ambalo lilikwama kwa muda mrefu kutokana na sababu za kisiasa na kiutendaji.
Ameeleza hayo leo katika mkutano wa adhara wakati akiomba kura kwa wananchi wa kata ya Kibeta ambapo uliudhuliwa na mamia ya wananchi,wakeleketwa na wanachama wa CCM wa jimbo jilo.
"Kwa heshima na taadhima nawaomba Oktoba 29 mwaka huu tumpe kura nyingi za shukrani Rais wetu ili aendelee kutekeleza miradi hii ya kimkakati aliyoianzisha na kutuletea mingine mipya ambayo itapandisha mara dufu maendeleo yetu" amesema Mutasingwa
Aidha akawakumbusha wanachi wa kata ya Kibeta kuwa miaka 20 nyuma walisema wanajaribisha upande mwingine wakamchagua diwani kutoka upinzani jambo ambalo liliwagharimu na kurudisha nyuma maendeleo yao mpaka mwaka 2020 walipofanya marekebisho na kuchagu diwani wa CCM.
Amesema kama kuonja sumu Kibeta waliishafanya hivyo kwahiyo waangalie kwa kipindi cha miaka mitano inayoisha ambapo walinchagua diwani Anastella Alphonce kupitia tiketi ya CCM ambaye ametekeleza miradi mbalimbali hususani hospitali,barabara ya Rugambwa-Kagambo na miradi mwingine ya kimaendeleo.
Amewaomba wananchi wa jimbo hilo kuchagua (CCM) katika uchaguzi wa mkuu mwaka huu ili kutatua changamoto ikiwemo kumaliza na kujenga miundombinu mipya ya barabara ili wananchi waweze kusafiri na kusafirisha bidhaa zao kwa usalama zaidi.
Amesema tatizo la Barabara kwa uwezo wa kitaalam alionao na ushirikiano kati yake na waandisi wengine wa Serikali na wa binafsi kero ya barabara inakwenda kuwa historia katika jimbo la Bukoba mjini hivyo, akawaomba wananchi kuchagua CCM ili kufanikisha ahadi hiyo.
Aidha akawashauri wanachama wa chama hicho kuendelea kudumisha umoja na mshikamano kati yao wakati huu wa kampeni na uchaguzi kwasababu hiyo ndiyo nguzo muhimu ya kuleta ushindi na maendeleo yao yatakuja ndani ya muda mfupi.
"Tusiposikilizana na kuanza kutengana tujue maendeleo yatakuwa ni changamoto kupatikana pia, maendeleo ya Bukoba mjini yanakua taratibu kutokana matokeo ya kupiga kura chache kwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunapaswa kutambua maendeleo ya kweli yapo ndani ya CCM tumpe kura za kishindo Dk.Samia ifikapo Oktoba29 mwam huu" ameeleza Mutasingwa
Amesema chama hicho kina Ilani hivyo yanayoahidiwa na wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya Taifa hadi kata siyo uongo bali ni mikataba kati ya wananchi na chama hicho kwahiyo ni lazima yatatekelezwa.
Amesema siasa za propaganda hazina nafasi tena katika jimbo hilo kwani maendeleo ya kweli yanapatikana CCM
Naye diwani wa Kata ya Kibeta Anastella Alphonce amewaomba wananchi kumpa ridhaa tena ya kuongoza miaka mitano mingine kwasababu miaka mitano iliyopita alikuwa darasani akijifunza, sasa anaenda kufanya makubwa kwa kushirikiana na mbunge wa CCM na Rais Dk Samia.