BUWASA Wakamilisha Mradi wa Maji Wenye Thamani ya Bilioni 3.1 Bukoba, Kuhudumia Wananchi 18,000

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba: Mamlaka ya Maji safi Na usafi wa mazingira Bukoba BUWASA wamekamilisha utekelezaji wa mradi wa maji ambao umegharimu Bilioni  3.1 ambao utanufaisha wananchi zaidi ya  elfu 18,000 wa kata tano za manispaa ya Bukoba na moja Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera 


Mratibu wa Mradi  huo  Daudi Byeyanga akitoa taarifa ya kukamilika kwa mradi huo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amesema kuwa mradi huo ulianza  kutekelezwa  mwaka 2020 na kusema  kuwa mradi huo  mekamilika kwa asilimia Mia moja 

Amesema huo ni mradi ambao unaenda kuondoa Adha kwa wananchi wa kata za pembezoni  mwa Mji wa Bukoba ambazo zilipata maji kwa mgao na kata nyingine kutoka Halmashauri  ya Bukoba ikiwemo kata  Kahororo,Buhembe  Nshambya ,Kashai na Nyakato

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya miradi ya  maji na vyanzo vya maji Ili miradi hiyo iweze kudumu muda mrefu.

Amesema serikali itahakikisha Kila mwananchi anayeishi mjini  anaunganisha maji Nyumbani kwa bei nafuu na mwananchi anayeishi kijijini Anatetembea mita 400 tu kufata maji.

Swaum Seveline ni mmoja wa wanawake wa kata ya Buhembe ulipojengwa mradi huo ameishukuru Serikali kuleta mradi huo maana umekuwa mkombozi kwao kwasababu walikuwa wakipata changamoto ya kufuata maji kwenye vijito vya asili ambavyo hutumiwa na wanadamu na mifugo.

"Maji ni maendeleo kwasasa hatupotezi muda mwingi kufuata maji umbali wa kilomita 16 watoto walipotumwa kufuata maji walitembea saa mbili na zaidi sasa tunatumia maji safi na salama karibu na makazi yetu, ukilinganisha na huko nyuma ambapo tulifua nguo mara moja kwa mwezi hari iliyosababisha kuliwa na chawa kutokana na uchafu "amesema Swaum.









Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top