Waziri Kikwete Ashiriki Uzinduzi wa Maonesho ya 49 ya Wakulima -Nanenane

0


 Na Ghati Msamba

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, ameshiriki katika uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 49 ya Wakulima, maarufu kama Nanenane, yaliyozinduliwa katika Viwanja vya 77 vilivyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo yamezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na yamewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, biashara, na viwanda kutoka ndani na nje ya nchi. Washiriki wametoka kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo China, India, Malaysia pamoja na nchi kadhaa za Ulaya, Afrika na Asia.

Katika ziara yake ya kutembelea mabanda ya maonesho, Rais Dkt. Mwinyi aliambatana na mwenyeji wake, Waziri Ridhiwani Kikwete, kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu. Akiwa katika banda hilo, Rais alipata fursa ya kujionea kazi mbalimbali zinazotekelezwa, zikiwemo teknolojia za TEHAMA zilizobuniwa na vijana wa Kitanzania kwa ajili ya kusaidia kutambua athari za mabadiliko ya tabianchi. Pia alioneshwa mfumo maalum wa kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto, kama sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na majanga.

Aidha, Rais Mwinyi alijionea mafanikio ya uwekezaji kupitia banda hilo, ikiwemo uzalishaji wa sukari kutoka Kiwanda cha Mkulazi – kiwanda kinachoendeshwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (NSSF) na Kampuni Tanzu ya SHUMA inayomilikiwa na Jeshi la Magereza.

Katika kufunga ziara yake, Rais Mwinyi alikabidhi zawadi kwa washiriki, wadhamini na washindi mbalimbali walioshinda kwenye vitengo tofauti vya uzalishaji mali, kama ishara ya kutambua mchango wao katika maendeleo ya sekta ya kilimo na viwanda nchini.

Wakati huo huo, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, tunapenda kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano ya kuahirisha kwa muda tukio la Msoga Marathon ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika tarehe 12. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa, hasa kwa washiriki na wadau waliokuwa tayari wamejiandaa kushiriki katika siku hiyo.

Tunaendelea na maandalizi ya kuhakikisha kuwa tukio hili linafanyika kwa ubora unaostahili katika tarehe mpya itakayotangazwa hivi karibuni. Msoga Marathon litaendelea kusimamiwa kwa viwango vya juu kama ilivyopangwa awali, kwa lengo la kuhamasisha afya, michezo na mshikamano wa kijamii.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top