Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limepongezwa kwa ubunifu wa kuzalisha nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes.
Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 6 Julai,2025 na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira),Mha. Cyprian Luhemeja alipozuru Kijiji cha STAMICO na Wadau Wake katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) jijini Dar es Salaam.
Ameahidi ofisi yake kuipa ushirikiano STAMICO ili gharama za uzalishaji wa nishati hiyo ziwe chini ili wananchi wengi kote nchini waweze kumudu kununua.
"Pia ofisi yangu itasaidia STAMICO kupunguza gharama zake za uzalishaji ili kuboresha usambazaji wa nishati hii kotè nchini",amesema.
STAMICO mezindua kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes kwenye maonesho haya.
Kampeni hiyo iliyopewa jina "Rafiki Briquettes Itembee" inawalenga wachoma nyama kwa hatua hii ya mwanzo na baadae itasambazwa kwa watumiaji wengine kama migahawa