Vijana 136 Wanufaika na Mafunzo ya Kidigitali Kupitia Mradi wa Inclucities Manispaa ya Ilemela

0


Na Angela Msimbira Mwanza

Mratibu wa Mradi wa  Green and smart Cities Bw. Ahamed  Sakib amesema jumla ya vijana 136 wamepatiwa mafunzo ya kutumia digitali kwenye kukuza biashara zao ili wanajikimu kiuchumi kupitia mradi wa IncluCities.

 Akitoa maelezo mafupi ya mradi wa IncluCities unaotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Bw.Sakib amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha vijana hkutumia teknolojia ya kidigitali katika kuendesha biashara zao na kujiongezea kipato katika dunia ya sasa inayotawaliwa na matumizi ya TEHAMA.

Anafafanua zaidi kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo vijana kujiajiri kupitia matumizi ya teknolojia kama vile mitandao ya kijamii, majukwaa ya kidijitali ya biashara na mbinu bora za usimamizi wa wateja mtandaoni.

"Mradi wa IncluCities una dhamira ya kuhakikisha hakuna kijana anayeachwa nyuma katika mapinduzi ya kidigitali. Vijana hawa 136 waliopatiwa mafunzo ni sehemu ya mkakati wa kuwainua kiuchumi na kuwasaidia kutumia digitali kama nyenzo ya mabadiliko ya maisha yao."amefafanua Bw.Sakib

Kwa mujibu wa Sakib, washiriki walipata elimu juu ya matumizi salama ya intaneti, uuzaji wa bidhaa mtandaoni (digital marketing), matumizi ya mitandao ya kijamii kibiashara, uandaaji wa maudhui bora ya kidigitali pamoja na mbinu za kulinda taarifa binafsi mtandaoni.

Aidha, Sakib amewataka vijana waliopatiwa mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia maarifa waliyopata kwa vitendo na kuwahamasisha vijana wengine katika jamii zao ili kuwe na wigo mpana wa ushiriki wa vijana katika uchumi wa kidigitali.

Mradi wa IncluCities unatekelezwa na shirika la Maendeleo la Ubelgiji kupitia Progam ya Green and Smart cities-SASA pamoja  na shirika la Trias, Enovet, VETA, TVET na VETA KIPAWA.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top