Uganda Yavutiwa na Mwenendo wa Biashara ya Madini na Mfumo wa Masoko Tanzania

0


Wizara ya Madini na Fedha ya Jamhuri ya Uganda imeonesha kuvutiwa na namna Tanzania inavyoendesha shughuli za biashara ya madini, hususan mfumo wa masoko unaotumika nchini, ikilenga kuboresha mifumo yao kwa kutumia uzoefu wa Tanzania kama mfano wa mafanikio.

Hayo yamebainishwa leo Julai 31, 2025 jijini Dodoma wakati wa ziara ya ujumbe kutoka Uganda uliofika katika Wizara ya Madini ya Tanzania ukiongozwa na Kamishna wa Madini wa Uganda Agnes Alabai kwa madhumuni ya kujifunza kuhusu mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa biashara ya madini pamoja na masoko ya madini nchini Tanzania.

Pia, ameipongeza Wizara ya Madini kwa kuwapatia mafunzo na taarifa mbalimbali zinazolenga kuboresha ufanisi wa sekta ya madini kwa kuzingatia uwazi bila kuficha taarifa yoyote.

Alabai amesema ziara hiyo imekuwa ni sehemu ya juhudi za Uganda kuimarisha sekta yake ya madini kwa kuiga mifumo yenye mafanikio kutoka mataifa jirani.

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Madini Tanzania, Dkt. AbdulRahman Mwanga, ameukaribisha ujumbe huo kutoka Uganda na kupongeza hatua yao ya kuamua kujifunza kutoka Tanzania ambapo amesema kuwa hatua hiyo inaonesha dhamira ya kweli ya kukuza na kuboresha sekta ya madini kwa njia ya ushirikiano wa kikanda na kubadilishana uzoefu.

“Tunafurahi sana kuona ndugu zetu kutoka Uganda wakiona umuhimu wa kujifunza kutoka kwa wenzenu hapa Tanzania. Hii ni ishara nzuri ya mshikamano wa kikanda na uelewa wa pamoja kwamba mafanikio katika sekta hii yanaweza kuimarishwa zaidi kwa kushirikiana,” amesema Dkt. Mwanga.

Aidha, Dkt. Mwanga amesema, Tanzania imefanikiwa kuanzisha na kuendesha mfumo wa masoko ya madini unaohakikisha uwazi, usalama na tija kwa pande zote zinazohusika, ikiwa ni pamoja na wachimbaji, wafanyabiashara, serikali na wanunuzi wa madini.

Naye, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini Vanance Kasiki amesema Tanzania imeendelea kuwalea na kuwainua wachimbaji wadogo ili kuweza kufanya shughuli za uchimbaji na biashara ya madini kwa  tija.

Pamoja na mambo mengine, Kisiki amesema Serikali kupitia Tume ya Madini ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Wizara.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top