Elimu: Fahamu Kanuni za Ubora wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira na Fidia Kwa Mteja Endapo Mita ya Maji Imeharibika

0


#MITA YA MAJI

Kanuni za ubora wa huduma za Maji na Usafi wa Mazingira( Ubora wa Huduma na Leseni za Mwaka 2020; Tangazo la serikali Na: 849, Viwango vya ubora wa huduma pamoja na gharama za fidia kwa kushindwa kufikia viwango vilivyowekwa. Kanuni ya 34(3) inazitaka mamlaka za maji zilizopewa leseni kufikia viwango vya kutoa huduma zitakazowajibika kulipa fidia kwa waathirika.

Kanuni za ubora wa huduma za maji na usafi wa Mazingira inaeleza kuwa endapo mita ya maji imeharibika, mamlaka inatakiwa kukarabati au kubadirisha mita iliyoharibika ndani ya siku 15 za kazi, mita iliyoharibika inapaswa kuwa imekarabatiwa au kubadirishwa tokea kutolewa kwa taarifa.

Endapo mtoa huduma atashindwa kufikia viwango vilivyowekwa, mtoa huduma atamlipa mteja shilingi 15,000.00 fidia ya msingi n shilingi 5,000 kwa kila siku inayoongezeka bila kupewa huduma.

Imeandikwa na Emmanuel Chibasa

Chanzo: ewura ccc

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top