Tanzania Kuwa Nchi ya Tatu Barani Afrika Uzalishaji Urani

0



●Utafiti wabaini akiba ya tani 54,000 za Urani

●Historia inasema kabla ya mwaka 1912 kiasi cha kg 400 za Mbale ya urani zilichimbwa na kusafirishwa

●Uzalishaji utadumu kwa kipindi cha miaka 12 kwa awamu ya kwanza

●Mradi kuvutia uwekezaji wa fedha za kigeni utakaofikia shilingi trilioni 3.6


Na.Samwel Mtuwa, URANI- Tanzania

Urani (Uranium) ni elementi ya kemikali yenye alama ya kikemia "U" na namba yake ya  atomia ni 92 katika jedwali la elementi. Aidha, Urani ni metali tekevu yenye rangi ya kijivu na nyeupe yenye mionzi ya usumaku.

Kitaalam madini ya Urani mara nyingi huonekana kwa wingi katika mifumo mbalimbali ya madini ambayo ni aina maalum za miamba au maumbo ya kijiolojia  kama vile uraninite, pitchblene , carnotite na Autunite.

Tafiti mbalimbali zilizofanyika zimeonesha madini ya Urani nchini Tanzania yaligundulika katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Namtumbo (Mkuju River), Bahi, Galapo, Minjingu, Mbulu,Simanjiro, Ziwa Natroni, Manyoni, Songea ,Tunduru, Madaba , na Nachingwea.

Japokuwa tafiti zinasema kuwa,  kabla ya mwaka 1912 kiasi cha kilogramu 400 za mbale ya urani zilichimbwa na kusafirishwa nje ya nchi ambapo toka kipindi hicho hakuna uchimbaji  mwingine uliofanyika.

Mradi wa utafiti na uendeshaji wa urani katika eneo la Mkuju River unamilikiwa na kampuni ya Mantra Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Urani ya Urusi (ARMZ) huku kampuni ya Uranium One Inc ndiyo waendeshaji wa mgodi huo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika katika eneo la mgodi wilaya ya Namtumbo mkoani Songea imebainika kuwepo kwa tani 54,000 za urani ambapo kulingana na akiba hiyo uzalishaji utafanyika kwa miaka 12  na kuvutia uwekezaji mkubwa wa fedha za kigeni (FDI) unaofikia zaidi ya shilingi trilioni 3.6. 

Tanzania itakapoanza uzalishaji kupitia Mradi wa Mkuju River Wilayani Namtumbo  itakuwa nchi ya tatu barani Afrika kwa uzalishaji wa madini ya urani baada ya nchi ya Niger yenye akiba ya tani 200,000 na Namibia yenye akiba ya tani 100,000 katika miradi yake mitatu ya uzalishaji.

Nchi ya Niger ndiyo nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa urani barani Afrika na ni miongoni mwa wazalishaji wakuu duniani.

Chanzo: Wizara ya Madini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top