NEMC Yaendelea Kutoa Elimu ya Mazingira Katika Maonesho ya SabaSaba

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali za mazingira katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Ikiwa leo ni siku ya nne tangu kuanza kwa maonesho hayo, NEMC inaendelea kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira, madhara ya uchafuzi wa mazingira, pamoja na kusisitiza wananchi, wawekezaji na wafanyabiashara kutekeleza matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Katika banda la NEMC, wananchi wanapata fursa ya kuuliza maswali na kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Baraza, na namna bora ya kudhibiti taka na kelele kwenye maeneo ya makazi na biashara.

Baraza linaendelea kuwakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake ili wapate maarifa sahihi yatakayowawezeshakuwa sehemu ya watetezi wa mazingira kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top