Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Sware Semesi ashiriki uzinduzi wa Jukwaa la kukutanisha wadau wa Mazingira nchini (Tanzania Green Summit) lililofanyika tarehe 04 July mwaka huu katika hotel ya Serena iliyopo Dar es Salaam
Akiongea katika uzinduzi huo, Dkt. Sware alisema "Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC),tunaipongeza timu nzima ya Tanzania Green Summit kwa kuleta jukwaa la kuwakutanisha wadau wote wa mazingira nchini, nasi tunaahidi ushirikiano kwa maendeleo endelevu ya Mazingira Nchini "
Ameongeza kuwa NEMC inatambua juhudi za jukwaa hilo katika kujenga sekta ya mazingira na inaahaidi kushirikiana nao katika mchakato mzima.