Polisi wa Kata ya Kasololo, Wilaya ya Misungwi, Mkoa wa Mwanza Mkaguzi wa Polisi Costantine Kuahidi ametoa elimu ya usalama barabarani kwa kikundi cha ngoma ya asili Bunungule, juu ya madhara ya kubebwa kwenye bajaji ya mizigo jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wao kwa kutumia bajaji ya mizigo kama chombo cha usafiri.
Aidha, amemuonya dereva wa bajaji kufuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani sambamba na kumtaka kuacha mara moja tabia ya kubeba abiria kwenye chombo hicho kwani kufanya hivyo ni kosa la kisheria linaloweza kusababisha ajali na madhara makubwa Kwa Maisha ya watu
Chanzo: Mtandao wa Polisi Tz