#UPATIKANAJI WA HUDUMA
Kanuni za ubora wa huduma za Maji na Usafi wa Mazingira( Ubora wa Huduma na Leseni za Mwaka 2020; Tangazo la serikali Na: 849, Imeeleza Viwango vya ubora wa huduma pamoja na gharama za fidia kwa kushindwa kufikia viwango vilivyowekwa. Kanuni ya 34(3) inazitaka mamlaka za maji zilizopewa leseni kufikia viwango vya kutoa huduma zitakazowajibika kulipa fidia kwa waathirika.
Tukiangazia upatikanaji wa huduma kwa mujibu wa viwango vya ubora vilivyoweka, Mamlaka zinatakakiwa kuunganisha huduma ya maji safi na mfumo wa maji taka kwa mteja katika kipindi cha siku 7 za kazi kuanzia pale malipo yalipofanyika.
Kanuni inaeleza kuwa mtoa Huduma atatakiwa kulipa fidia kwa kushindwa kufikia viwango vilivyowekwa, Kanuni inaeleza kuwa mtoa huduma atamlipa mteja shilingi 15,000.00 kama fidia ya msingi na shilingi 5,000 kwa kila siku inayoongezeka bila kupewa huduma.
✍️Imeandikwa na Emmanuel Chibasa
Chanzo: ewura ccc