Baadhi ya wananchi wa Musoma Mkoani Mara, Wametoa wito Kwa wakazi wa Mkoa wa Mara na maeneo mengine hapa nchini, Kuwachagua Viongozi Wenye Uwezo na vigezo Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Ili kupata Viongozi Bora wataosaidia kuleta Maendeleo na kutatua Changamoto zao.
Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wakitoa wito Kuhamasisha Wananchi Kushiriki Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Wamesema Wananchi wa Mkoa wa Mara na Tanzania Kwa ujumla, katika Kipindi cha uchaguzi wanapaswa kujitokeza Kwa wingi kusikiliza sera za wagombea watakaokua wameteuliwa na vyama vya Siasa, kisha kuchuja wagombea wenye uwezo na Vigezo ili kupata Viongozi wenye kiu ya kuwaletea wananchi Maendeleo na kushughulika na Changamoto zao
John Bwana, Musa Kerenge na Musa Mwambiga ni miongoni mwa wakazi Musoma, wanasema Kipindi cha uchaguzi wananchi wanapaswa kuwakataa Viongozi watoa rushwa, lakini pia kutowachagua Viongozi Kwa mihemko Ili kuwapata viongozi sahihi watakaoshiriki na kutatua Changamoto zinazo wakabili Wananchi Katika sekta mbalimbali Ikiwa ni pamoja na Elimu, Afya, miundombinu pamoja na kusaidia kutatua tatizo la ajira Kwa Vijana.
Bonyeza hapa chini kutazama na Kusikiliza👇👇
https://www.facebook.com/share/v/12JLwJBHhNw/?mibextid=jmPrMh