Viongozi wa Serikali Kagera Watakiwa Kufuatilia Mipango ya Kampeni za Afya

0


 Angela Sebastian-Bukoba

SERIKALI mkoani Kagera imewaagiza viiongozi wote kuanzia ngazi ya Wilaya hadi vijiji kuhakikisha wanafuatilia kikamilifu mipango ya kampeni za Afya zinazofanyika katika meneo yao, ili kufikia malengo ya Serikali ya kuhakikisha kila mtu anapata kinga hususani chanjo mbalimbali zinazotolewa na Serikali.

Aidha Amesema kuwa mkoa huo unapakana na nchi nyingi za Afrika Mashariki hivyo kupata maambukizi au magonjwa ya mlipuko kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni rahisi kama taratibu za kinga hazijafuatwa.

Hayo yameelezwa na mkuu wa Wilaya ya Muleba Abel Nyamahanga  alipomwakilisha mkuu wa mkoa huo Hajati Fatma Mwassa katika mafunzo ya siku moja kwa watumishi wa idara ya Afya wa ngazi mbalimbali na viongozi mbalimbali wa mkoa huo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa ambapo,aliwashauri wataalam wa idara ya Afya kuendeleza juhudi zao katika kuhamamsisha kazi zote za kinga hasa chanjo,usafi wa mazingira na mazoezi ya utayali kwa kukabiliana na milipuko ya magonjwa.

Pia amewashuari wataalama wa idara ya Afya mkoani humo kujiandaa kila mara juu ya magonjwa mbalimbali hususani ya mlipuko pindi unapojitokeza ili pawepo uimara wa kuhakikisha tunatafuta wadau wa kuongeza nguvu na kasi ya watumishi wanaofanya kazi ya uchanjaji,uhamasishaji pamoja na ufuatiliaji katika ngazi ya jamii.

“Viongozi sisi ni ukuta,tusipopambana kujenga ukawa imara ni rahisi kusambaza magonjwa kutoka sehemu  moja na kwenda nyingine mtakumbuka kuwa mkoa wetu wa Kagera tunapaka na nchi nyingi za Afrika mashariki pamoja na muingiliano mkubwa ya watu tulio nayo haiwezi kutuacha salama,hivyo inatupasa kila mara kujiandaa juu ya magonjwa ya mlipuko na majanga mbalimbali”ameeleza Nyamahanga

Amesema kufanya kazi kwa umoja,mshikamano na kujituma hasa wakati wa majanga kama vile magonjwa,kuhamasisha chanjo ni kujenga heshima ya Serikalia na mkuu wa nchi Dk. Samia Suluhu Hassan aliyeona viongoi haoa na watendaji wa ngazi zote wanafaa kuwa wasaidizi wake na kuwatuma katika maeneo hayo wanayoyaongoza.

Amewashukuru wadau wote wa Afrika kupitia washirika wake wa Amref na Msalaba mwekundu kwakuanza utekelezaji wa kuhamasisha na kuchagiza hari ya uhamasishaji wa utoaji wa huduma za chanjo katika maeneo yao.

Amesema Kampeni ya mtu ni Afya ikifanyika kwa usahii fedha itapatikana kwa wingi  kwa ajili ya kuimalisha Afya za wananchi kutoka kwa wadau mbalimbali pia amewashauri wananchi kutumia vyakula vinavyozalishwa  mkoani humo kufanya lishe bora na kuondokana na ugonjwa wa utapiamlo ambao unaendelea kutafuna mkoa huo sambamba na kujenga vyoo bora kwani nyumba ni choo.

Kwa upande wake Afisa Afya wa mkoa wa Kagera Yassin Mwinoli amesema mafunzo hayo ya siku moja yamelenga kutoa elimu kwa jamii kuwa upo utekelezaji wa zoezi la chanjo ambapo hatua ya uchanjaji katika mkoa huo ziwezekuzingatiwa kwa kiwango kikubwa  ili kuwalinda wananchi dhidi ya magonjwa yote yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya chanjo

“Tumeweka mikakati madhubuti na kukubaliana kwamba ifikapo Julai 30 mwaka huu tuweze kufanya tathimini ya mambo yote yaliyoelekezwa kufanyika kule ngazi ya nchini kwenye jamii hasa kutambua waliochanjwa ni wangapi?sababu za kuwafanya wengine wasichanjwe ni zipi?wako wapi?wangapi hawakuchanjwa?ambapo zoezi hilo linahusisha maafiasa tarafa wa mkoa huu,watendaji na wenyeviti wa kata,vijiji na vitongoji na wahuduma wa Afya ngazi za jamii”anaeleza Mwinoli

Amesema viongozi hao wanachokwenda kufanya ni kupita nyumba kwa nyumba na kubaini waliochanjwa na ambao hawakuchanjwa ambapo kufanya hivyo ni kuhakikhsa mkoa wa Kagera uko safi na salama katika kuwalinda wananchi ili wasiweze kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.

 Aidha amesema wataalama hao walipata mafunzo, miongoni mwa kazi wanazopaswa kuafanya ni kufuatilia magonjwa ya mlipuko,ukaguzi wa maeneo yote ya vyakula,kusajiri maduka ya vyakula ukaguzi wa shule usimamizi wa usafi wa mazingira kwa kina na kuhakikisha wanatoa elimu ya Afya ya jamii sehemu zote ili wananchi wawezekupata ulewa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top