Na Angela Sebastian
Mjumbe mkutano mkuu wa Taifa anyeiwakilisha Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Khald Mussa Nsekela amechukua fomu kuomba kuteuliwa na CCM kugombea ubunge jimbo la Kyerwa.
Nsekela baada ya kuchukua fomu amesema lengo la kuchukua fomu na kugombea jimbo hilo ni kuchochea maendeleo katika jimbo pia,kuwa yeye ni kada wa Chama hicho hivyo aliona ni vyema kutumia haki yake ya kikatiba ili akifanikiwa aweze kutoa mchango wake katika kulitumikia chama na wana Kyerwa.