NEMC Yashiriki Uzinduzi wa Daraja la Magufuli (Kigongo-Busisi) Yatoa Wito Kwa Wananchi Kuhifadhi Mazingira

0


👉Yatoa wito Kwa Wananchi Kigongo-Busisi Kuacha Mita 60 toka Kwenye kingo za ziwa

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) ni miongoni mwa Taasisi zilizoshiriki katika uzinduzi wa Daraja la Magufuli (Kigongo Busisi) Mkoani Mwanza Wilaya ya Misungwi alililozinduliwa rasmi leo 19 Juni, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naye Mtendaji Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini  ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa  kufanikisha ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi linalounganisha Mkoa wa Mwanza na Mikoa mingine kama Geita na Kagera pamoja na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.

Aidha, Semesi ameongeza kuwa daraja hilo litafungua fursa za Kiuchumi na Kijamii na amehimiza utunzaji wa miundombinu na Mazingira katika eneo la Kingongo-Busisi.

" Ninatoa wito kwa wananchi wote hususani katika hili eneo la Kigongo- Busisi kuacha mita sitini toka kwenye kingo za Ziwa, kuepuka kutupa taka ngumu na taka maji kiholela, kuhakikisha wananchi wanazingatia misingi ya kilimo endelevu ili kupunguza uchafuzi kwenye Ziwa" alisema Dkt. Semesi. 

Naye Meneja wa Kanda ya Ziwa - NEMC  bwana Jarome Kayombo amesisitiza miradi yote inayofanyika ndani na kando ya Ziwa ihakikishe inafanya Tathimini ya Athari kwa Mazingira (EIA) kabla ya kuanza kutekeleza miradi husika ili kupunguza uharibifu wa Mazingira hasa katika eneo la Ziwa. Kayombo amewaasa watanzania wote watakaotumia daraja la Kigongo - Busisi kulinda miundombinu ya daraja na kuacha kutupa taka ziwani ili kulinda mifuko ikolojia ya Ziwa.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top