Na Angela Sebastian-Bukoba,
Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera ((JWT) imesema kuwa, bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026 iliyosemwa Bungeni na Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba imetoa ufumbuzi wa baadhi ya kero zilizoondoa utulivu wa kubiashara na kudhoofisha mitaji.
Hayo yameelezwa na leo mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa huu Nicholaus Basimaki ambapo ameipongeza jitihada za Serikali maana bajeti imegusa maeneo mengi ya wafanyabiashara na itapunguza kero kwao.
“Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ameelekeza wasaidizi wake waweze kusikiliza changamoto za wafanyabishara ambapo tumeona kwenye bajeti yameainishwa mambo mbalimbali mfano sheria ya fedha ya serikali za mitaa sura ya 290 ambayo ni hotuba kupitia Waziri wa fedha inapendekeza ifanyiwe maboresho”amesema Basimaki
Ameeleza kuwa, wafanyabiashara wanaunga mkono kwamba katika maeneo hayo hasa kwenye maeneo ya tozo na ushuru mfano ushuru wa huduma (service lev) ambayo ilikuwa ikitozwa kwenye mauzo ghafi 0.3 kama itakwenda kutozwa kwenye faida kwa maana ya pato ghafi itasaidia.
Ametaja eneo jingine lililopewa unafuu ni kwenye hotel lev (ushuru wa hotel) ambao ulikuwa unakokotolewa kwenye mauzo baada ya kuondoa matumizi unatoa sasilimia 10 na hii itaondoa kero kwa wawekezaji wa hotel, nyumba za wegeni na wafanyabiashara.
“Ilikuwepo kero ya wafanyabiashara kufungiwa maduka bila kusubili mtu anafika anafanya ukaguzi hapo hapo anafunga maduka sasa na tunaona pendekezo hili likipitishwa kwenye mswada wa sheria itasaidaia kuondoa kero ambazo zitaweza kuongeza tija na mazingira mazuri ya ufanyaji biashara, wafanyabiashara watajiamini na watakuwa na muda wa kufanya bishara bila mawazo ya kufungiwa na sisi tunasema mapendekezo haya yapitishwe na mswada huu usainiwe iwe sheria” amesema Basimaki
Amesema wanakubaliana na mapendekezo ya Waziri wa fedha kwenye mswada wa sheria ushuru wa kupakia na kushusha ufutwe kama ilivyopendekezwa na katika misamaha iliyotolewa kwenye mali ghafi/bidhaa za kuongeza uzalishaji pia mapendekezo hayo yaendelee.
Pia ameiomba serikali kutatua changamoto moja ya kwenye maji kwani walitegemea tozo ya inayotozwa kila lita ya maji sh. 46 ipunguzwe hadi sh.10 ili kuwezesha viwanda vya maji hasa vidogo kuendelea kuongeza uzalishaji ili waendelee kushindana na viwanda vikubwa.
Naye Ramadhan Makule ni mfanyabiabaishara wa mazao na mmiliki wa hotel Wilayani Ngara mkoani hapa amesema kuwa, bajeti ya Serikali imeonyesha kuwajali wafanyabiashara kwani malalamiko yao kwa asilimia kubwa yamefanyiwa kazi.
Aidha amewashauri,wabunge ambao ndiyo wako karibu na jamii waone kile ambacho hakijaguswa na Serikali wasemee ili wafanyabiashara waendelee kupata unafuu maana wafanyabiashara wana nafasi kubwa kwani wanaongeza kipato cha nchi kupitia kulipa kodi.
“Serikali haiwezi kuendeshwa wakati wafanyabiashara wanalalamika lakini wafanyabiashara wakifurahi mambo yatakuwa mazuri tutalipa kodi na hakuna kitu ambacho kitakwama” amesema Makule
Akizungumzia wawekezaji/wafanyabiashara wa nje ya nchi amesema kuwa, katika bajeti wameangaliwa Wachina waliopo Kariakoo pia mkoa wa Kagera maeneo ya mpakani wafanyabiashara wengi wanafanya baishara za mazao.
"Wafanyabiashara kutoka nje mfano Rwanda, Burundi na nchi nyingine wanaingia kwetu wanafanya biashara wakati watanzania hawawezi kutoka nje ya mpaka kwenda katika nchi hizo kufanya biashara kwani sheria ya nchi hizo haiwaruhusu mpaka wanunulie mpakani lakini wanaotoka nchi jirani wanaingia hapa nchini kila sehemu ma wanafanya biashara zao"ameeleza Makule kwa uchungu
Hivyo akaomba serikali isiangalie sehemu moja ya Wachina bali iangalie pande zote za wafanyabiashara na waone wafanyabiasha wa ndani wanawalindaje kuweza kufanya biashara zao za mazao na biashara nyingine ndogo ndogo.
Kwa upande wake Sarah Sevelian mfanyabiashara wa wa duka la nguo mjini Bukoba ameishukuru serikali katika bajeti iliyosomwa kwa kulenga kutatua changamoto za wafanyabiashara kwani walikuwa na kero ya kufungiwa biashara zao.
"Naami kwa bajeti hii iliyosomwa inaonyesha kuwa sheria inayowapa mamlaka serikali za mitaa itaondolewa tutafanya biashara zetu bila usumbufu"amesema Sevelian
Amesema serikali iendelee kutatua changamoto za wafanyabiashara ili kuweka unafuu kwao wa kuweza kufanya shughuli zao kwa haki na kujiamini.