SMAUJATA Mara Yaanza Ziara Kutoa Elimu ya Ukatili wa Jinsia na Maadili Katika Shule za Msingi na Sekondari

0



Na Shomari Binda

KAMPENI ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii( SMAUJATA) mkoa wa Mara imeanza ziara ya kupita kwenye shule za msingi na sekondari ikiwa na lengo la kutoa elimu Kwa wanafunzi

Elimu inayotolewa ni masuala ya ukatili wa kijinsia,namna ya utoaji wa taarifa kwa watoto wanaofanyiwa vitendo hivyo na uhimizaji wa maadili mema.

Katika siku ya kwanza mei,28,2025 kampeni hiyo imefika shule ya msingi Kambarage A na B na kufikisha elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Akiwa shuleni hapo Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Mara Joyce James, alitoa mada kuhusiana na mitandao salama kwa watoto na kuwaeleza wanafunzi wanapotumia simu za wazazi na walezi watumie kwa kupata elimu na sio mambo yasiyofaa.

Amesema mirandao isiyo salama inachangia mmomonyoko wa maadili na kuzalisha kizazi kisichofaa na yapo mambo mazuri yanayofaa kwenye mitandao wanayopaswa wanafunzi kuyatumia.

" Tunawashukuru walimu kwa kutupokea vizuri shuleni hapa na tumekuja kutoa elimu kwa wanafunzi kwa masuala mbalimbali yakiwemo ya maadili mema kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na matumizi mazuri ya mitandao.

"Nimekuja na wenzangu Mwenyekiti wa  Idara ya Uenezi na Uanachama mkoa  shujaa Masatu Robert pamoja na mkuu wa idara ya elimu mkoa shujaa Lena Enock kwa kutambua uzalendo na umuhimu wa Taifa letu tumefika shule za msingi Kambarage A/B zilizopo kata ya Bweri Wilaya Musoma ili tutoe elimu ya Ukatili wa kijinsia,mmomonyoko wa maadili na Mtandao salama kwa mtoto.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amemshukuru Katibu Tawala wa Wilaya ya Musoma Ally Mwendo kwa kuwezesha usafiri unaosaidia kufanya kampeni hiyo huku walimu wa shule hizo wakionyesha kufurahishwa na kampeni hiyo pamoja na kazi inayofanywa na mashujaa wa SMAUJATA mkoa wa Mara.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top