Shiriki Katika fursa ya Mpango Maalum wa Kuendeleza Wajasiriamali wa Afreximbank 2025 kwa Wajasiriamali wa Kiafrika ambao unatoa Fedha hadi $250,000)
Benki ya Afreximbank inakaribisha waombaji kwa mpango wake mkuu wa kukuza biashara (Flagship Accelerator Program) kwa mwaka 2025. Mpango huu unalenga kuwasaidia wajasiriamali wa Kiafrika walio na maono makubwa na teknolojia zinazoweza kupanuka, ili kushughulikia changamoto kubwa katika maeneo yafuatayo:
Malipo ya mipakani (cross-border payments)
Ufadhili wa biashara (trade finance)
Mifumo ya biashara mtandaoni (digital commerce platforms)
Faida kwa Washiriki:
Uwezekano wa kupata fadhili hadi dola za Kimarekani 250,000 ($250,000)
Mafunzo ya kina na ushauri kutoka kwa wataalamu Kupanua mtandao wa kibiashara barani Afrika
Uungwaji mkono katika kuendeleza na kupanua suluhisho la kiteknolojia.
Vigezo vya Kushiriki:
Mwombaji awe mwanzilishi au timu ya waanzilishi wa biashara yenye suluhisho linalohusiana na malipo ya mipakani, ufadhili wa biashara au biashara za kidijitali.
Biashara iwe na uwezo wa kupanuka (scalable) na suluhisho lake liwe linashughulikia changamoto halisi barani Afrika.
Uwe na rekodi nzuri ya maendeleo ya mradi au teknolojia.
Maelezo Zaidi na Jinsi ya Kutuma Maombi:
Tembelea: https://opd.to/3Ssfj5d