Ukeketaji Sio Mila ya Kujivunia - Mhe.Edward Gowele

0


Na Magdalena Nkulu WMJJWM- Tarime Mara

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Edward Gowele amesema ukeketaji ni mila isiyotakiwa kuendelezwa katika jamii yoyote kwani ni mila kandamizi kwa watoto wa kike.

Gowele ametoa kauli hiyo Julai 29, 2026 katika kijiji cha Nyamongo, wilayani Tarime wakati akihitimisha msafara wa kusambaza Mkakati wa Kitaifa wa Kisekta wa Kutokomeza Ukeketaji.

“Ni kitendo cha ukatili wa kijinsia, natoa wito kwa makundi yote kuendelea kuwa mabalozi wa kupinga ukeketaji na nawasihi Wahanga kuacha kukaa kimya, watoe taarifa kwenye mamlaka husika” amesema Gowele.

Aidha, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kulinda haki za watoto nchini na kuhakikisha ukatili wote unatokomezwa.

Akitoa taarifa ya msafara huo uliopita kwenye mikoa mitano, mratibu Dennis Moses amebainisha kwamba, lengo la Mkakati huo ni kuhakikisha ukeketaji unatokomezwa kutoka asilimia 8 ya sasa hadi kufikia asilimia 4 mwaka 2030.

Akitoa tamko kwa niaba ya Wazee wa Kimila wa mkoa wa Mara, Mzee Giliud amasema wazee wa Mila wameendelea kupata elimu na kwamba, watahakikisha wanahamasisha wananchi kuachana mila hiyo mkoani hapo kwani inadidimiza ndoto za wasichana wengi.

Nao baadhi ya wananchi wilayani Tarime akiwemo Ngariba aliyeacha vitendo hivyo Anitha Nyangi,

amesema ni ukatili sana kwasababu wasichana wanaofariki wakati wa ukeketji wanatupwa na anatelekezwa porini bila msaada wowote.

Msafara huo ulihusisha Wataalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, wadau wa maendeleo kutoka Shirika la UNFPA pamoja na mashirika ya kijamii ya “Hope for Girls and Women” na Sauti ya Jamii, umefanikiwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali na kuwafikia wananchi 6,370 katika Halmashauri 6 za Chemba, Karatu, Mbulu, Singida, Serengeti na Tarime kuanzia Julai 19 hadi 29, 2026.

✍️maendeleo ya jamiu











Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top