NHC Yatakiwa Kutoa Taarifa ya Fursa za Kibiashara kwa Wananchi

0


Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetakiwa kuwapa taarifa wananchi juu ya fusa za kibiashara zitakazofanyika katika miradi mbalimbali linayoitekeleza nchini kote ili wachangamkie fursa zinazopatikana kupitia miradi hiyo ili kujiletea maendeleo.

Akizungumza mkoani Tabora wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Kibiashara la Tabora Biashara Complex lenye thamani ya zaidi ya a Bilioni 4.1 liliopo mtaa wa Gonguini mkoani humo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya amesema shirika hilo linapaswa kufanya kazi kwa uwazi kwa kuishirikisha jamii kikamilifu jamii ikiwemo kuwajulisha gharama za upangaji kwenye mradi huo.

Mhe. Mmuya amesisitiza pia ni wajibu kwa shirika hilo kutoa taarifa kwa walengwa juu ya miradi yake ya kimkakati kwa kuwapa elimu ya kutosha kuhusu ubora wa mradi husika.

Vilevile, Naibu Waziri Kaspar Mmuya amelitaka Shirika hilo kuhakikisha kuhakikisha linatoa haki sawa kwa kila mwananchi kupata fursa ya kumiliki nyumba ndani ya miradi hiyo pasipo upendeleo wowote.

Ameongeza kuwa shirika linapaswa kuzalisha miradi inayogusa wananchi wa kawaida nchini ili waweze kupata fursa ya kumiliki nyumba hizo zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Kadhalika Naibu Waziri Kaspar Mmuya ametoa wito kwa Shirika la Nyumba la Taifa kuanzisha viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi ili kutanua wigo kwa kibiashara wa shirika hilo na kujiongezea thamani.

Ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 55 baada ya kukamilika kwake litachangia kuimarisha uchumi wa shirika, kuongeza mapato ya Mkoa wa Tabora na taifa kwa kiujumla.

Aidha, kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tabora Bi. Upendo Wella kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Bw.Paul Chacha, ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kuchangamkia fursa zilizopo katika mradi huo kwakuwa wao ndio kipaumbele muhimu cha kwanza.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama watahakikisha mradi unatekelezwa kwa ubora ili kumnufaisha mwananchi ambaye ni mkazi wa Tabora.

chanzo wizara ya ardhi

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top