Wizara ya Elimu Tafuteni Fedha kwa Ajili ya Ujenzi wa Bweni na Nyumba za Walimu - Dkt. Nchimbi

0


 

Na Angela Sebastian 

Makamu wa Rais balozi Dk.Emmanuel Nchimbi amemwagiza waziri wa Elimu Prof.Adlof Mkenda kuhakikisha anatatua changamoto za upatikanaji wa fedha za ujenzi wa bweni la wavulana na nyumba za walimu  katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam tawi la Kagera.

Dokta Nchimbi amesema hayo wakati akiwa mgeni rasmi  katika halfa ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam Kanda ya Kagera kilichopo vijiji vya Itahwa na Kangabushalo kata Karabagaine katika Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera 

Amesema kuwa  ujenzi wa mradi huo uliopo  chini ya mradi wa elimu ya juu kwa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) unatekelekelezwa katika mikoa yote nchi nzima ili kuwezesha idadi kubwa ya vijana wanapata elimu ya bora ya kuwawezesha wanakuwa na ujuzi wa kuwakwamua kiuchumi tofauti na ilivyokuwa huku nyuma .

Dokta Nchimbi amesema kuwa ujenzi wa chuo hiki ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika  kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya mkoa wa Kagera na Taifa kwa ujumla huku akisema kuwa serikali ya awamu ya sita ya dk. Samia Suluhu Hassan inafuatilia kwa umakimi ujenzi wa chuo hicho katika kuakikisha kinakamilika Kwa wakati ili kufikia malengo yake 

Ameagiza ungozi wa chuo hicho kuhakikisha mitaala inayotolewa inaendana na utolewaji wa elimu ya amali itakayomwezesha, wanafunzi anapohitimu katika chuo hicho anaweza kujiajiri na kukitegemea pasipo kusubiri kuajiliwa ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya kazi nchi yoyote hususani katika nchi za Afrika Mashariki.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha UDSM Rais mstaafu wa hawamu ya nne Dk.Jakaya Mlisho Kikwete akitoa salaam chuo hicho kwa mgeni rasmi amezitaja fursa za kiuchumi na uwekezaji mkoani hapa ambazo zinaenda kuletwa na chuo hicho ambazo ni kukuza uchumi wa kuongeza ajira.

Aliwataka viongozi wa mkoa wa Kagera kuongeza ukubwa wa eneo lingine nje ya lililopo sasa kwa ajili ya ujenzi endelevu wa baade kwasababu mikakati ya UDSM ni kuhakiisha tawi hilo linakuwa chuo kikuu kinachojitegemea.

Naye makamu mkuu wa chuo prof.William Anangisye alisema ujenzi wa mradi huo ni kutokana na maono ya Rais Dk.Samia kuhakikisha Watanzania wengi wanafikiwa na elimu ya juu kupitia ubora wa mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia ambapo amesema kuwa mpaka ujenzi wa chuo hicho unakamilika jumla ya   kiasii cha shilingi bilioni 14 zitatumika na mpaka sasa zaidi ya shil bili.6.6 zimeishalipwa kwa wakandarasi.











Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top