TISEZA na JKCI Kushirikiana Katika Kuhamasisha Uwekezaji Kwenye Sekta ya Afya Nchini

0


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Bw. Gilead Teri amesema kuwa lengo la ushirikiano kati ya TISEZA na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ni kutumia uzoefu na huduma za kisasa zinazotolewa na JKCI kama kichocheo cha kuvutia wawekezaji zaidi katika sekta ya afya.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge, ameongeza kuwa taasisi yake ina imani kubwa kuwa TISEZA itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuvutia wawekezaji watakaoshirikiana na JKCI kuwekeza katika ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo. 

Ushirikiano huu sio tu utaboresha hali ya uwekezaji nchini bali pia utasaidia katika utoaji wa huduma bora na za kitaalamu zinazopatikana kwa urahisi zaidi kwa wananchi wote.

Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top