NEMC Yashiriki Kikao cha Teknolojia za Urejeshaji Mazingira Nchini Austria

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikao cha kutathmini mapungufu na changamoto za teknolojia za kimazingira zinazotumika kwenye kurejesha mazingira yaliyoharibiwa au kuchafuliwa (remediation technologies).

Kikao hicho kilifanyika katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Nyuklia (IAEA) yaliyopo jijini Vienna, Austria kuanzia tarehe 13-17 Oktoba, 2025.

Lengo la kikao ni kukutanisha wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wanaohusika na Udhibiti na Tafiti katika Sekta ya Nishati ya nyuklia ili kujadili njia bora za urejeshaji wa mazingira yaliyoharibiwa au kuchafuliwa.

Njia mbalimbali za urejeshaji wa mazingira zilijadiliwa na nchi wanachama pamoja na mapungufu na changamoto zake na kujifunza njia bora inayoweza kutekelezwa na nchi husika

Chanzo: NEMC



Chapisha Maoni

0 Maoni
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Chapisha Maoni (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top