Na Angela Sebastian
Karagwe : Mgombea ubunge wa jimbo la Kyerwa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Khaldi Mussa Nsekela amemshukuru Dk. Samia Suluhu Hassan
kwa kutoa shilingi bilioni 84 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Kyerwa tangu alipoingia madarakani.
Nsekela ametoa shukrani hizo leo katika mkutano mkubwa wa kunadi Ilani ya CCM na kuomba kura za mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan uliofanyika uwanja wa Kayanga Wilayani Karagwe.
Amesema Dk.Samia hana deni kwa wana Kyerwa bali wao ndio wanapaswa kulipa shukrani kwa kumpigia kura nyingi ifikapo Oktoba 29 mwaka huu.
"Wanakyerwa wanasema wanasubiri wakati ufike wakupigie kura za kutosha kutokana na sababu zifuatazo ambazo ni pamoja na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya Elimu,Afya,maji na Umeme ambayo imegharimu sh.bil 84 na kupanda kwa bei ya zao la kahawa kutoka sh.1000 hadi 8000 kwa kilo"anasema Nsekela
Anasema Ilani ya CCM imesheheni mambo mengi mazuri yanayomgusa kila mwananchi hivyo wanakyerwa wana imani Dk Samia anaendelea kutekeleza yote aliyoyaaahidi ili wananchi wake waendelee kunufaika na matunda ya nchi yao.

.jpg)
.jpg)





.jpg)


