Je unafahamu nini Kuhusu Utoroshwaji wa Fedha kwa Njia Haramu / Illicit Financial Flows?

0


Nafahamu katika harakati zako za maisha unaweza kuwa na ufahamu kuhusu utoroshwaji kwa fedha kwa njia haramu au kwa lugha ya kingereza Illicit Financial Flows lakini pia natambua pia wapo baadhi ya watu hawana uelewa kuhusu jambo hili.

Kwa mujibu wa taasisi ya PolicyForum kupitia ripoti ya muhtasari wa kisera kuhusu mitiririko Haramu ya Fedha (IFFs): Mzigo kwa bajeti ya Taifa ya Tanzania, mitiririko haramu ya fedha (IFFs) inamaanisha uhamishaji wa fedha au rasilimali zilizochumwa au zilizohawilishwa au zilizotumika kiharamu nje ya mipaka yanchi.

Mitiririko haramu ya fedha (IFFs) ipo katika miundo tofauti tofauti kutokana na shughuli za kibiashara au /na za kihalifu. Hizi ni pamoja na uepukaji kodi, ukwepaji kodi, upotoshaji wa bei ya biashara/ bidhaa, uhawilishaji wa matumizi mabaya ya bei (transfer pricing abuse), rushwa, utoroshaji wa mitaji, biashara ya madawa ya kulevya, biashara ya wanadamu, magendo, biashara ya silaha na utakatishaji fedha. Hii mitiririko hukausha rasilimali muhimu kutoka serikalini, na kupunguza fedha zinazohitajika kuendeleza sekta muhimu kama elimu, afya, na kilimo, hivyo kuathiri kwa viwango tofauti makundi ya pembezoni katika nchi zinazoendelea kama Tanzania.

Naye mwenyekiti wa bodi ya Policy Forum Israel Ilunde akizungumza katika mahojiano na kituo cha Clouds Fm kuhusiana na mada hii alieleza kuwa, Utoroshaji wa fedha kwa njia haramu ni vitendo ambavyo vinafanyika kutembeza fedha na rasilimali za umma na kwanza zinapatikana kiharamu, zinasafirishwa kiharamu na zinatumika kiharamu kwa njia ambazo hazifai.

Mwendelezo wa Mitiririko Haramu ya Fedha (IFFs) inachochewa na mtandao wa mapungufu ya kimfumo, hivyo kuruhusu fedha kupotea kupitia mianya katika uchumi wa kitaifa bila kugundulika.Kiini hasa cha tatizo ni taasisi zisizo imara na mifumo dhaifu ya udhibiti, ambapo utekelezaji usio na tija na ukosefu wa uwazi na uwajibikaji hutengeneza fedha haramu kuhamishwa bila kugundulika. hasa katika sekta zilizo na rasilimali kubwa kama vile madini. 

Hapa makampuni hunyonya kupitia mianya katika udhibiti - kuripoti mapato duni, kutoa thamani ndogo ya mauzo ya nje, na kubadilisha kwa werevu bei ya uhawilishaji ili kuhamisha faida Kwenda nchi za nje. Haya mazoea yasipodhibitiwa hukausha mapato ya taifa na kuibia serikali rasilimali zinazohitajika sana kwa huduma za jamii.

Nje ya mipaka ya nchi, usiri wa fedha duniani, una sehemu nyeti katika suala hili. Nchi zenye sheria kali za usiri ni maeneo mazuri sana kwa fedha haramu, watu binafsi na makampuni hulindwa dhidi ya uchunguzi kiasi kwamba ni vigumu sana kufuatilia fedha zilizoibwa.

Uendelevu wa mitiririko haramu ya fedha (IFFs) ni zaidi ya tatizo la kiuchumi ni mgogoro wa kidunia. Hudunisha maendeleo, huongeza ukosefu wa usawa na kumomonyoa misingi ya uhuru wa kiuchumi. Bila kudhibitiwa, hii mitiririko ya utajiri unaowezekana (potential) na hali halisi inayotokana na unyonyaji wa fedha.

Chanzo: Policy Forum

✍️Imeandikwa na Emmanuel Chibasa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top