Wazazi na Walezi Watakiwa Kuangalia Upya Malezi ya Watoto Bukoba

0


 Na Angela Sebastian 

Bukoba : WAZAZI na walezi mkoani Kagera wametakiwa kuangalia upya malezi ya watoto na kuongeza umakini hasa wakati huu ambapo vitendo wa unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto vimekuwa tishio kwa Taifa letu.

Serikali inajitaidi kutafuta njia mbalimbali za kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa na wahusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Hayo yameelezwa na  Leila Shelali ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la siku moja lililoendeshwa na mtandao wa Chama Cha Wanafunzi  na Vijana Waislam Tanzania (TAMSYA) kiislam mkoa wa Kagera katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya Bukoba mjini Bukoba na kuhudhuliwa na watoto, vijana ,walimu ,wazazi na viongozi mbalimbali wa dini,Serikali.

Shelali amesema lengo kuu la kongamano hilo ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa maadili yanayoendana na mafundisho ya kidini,kuishi uhadilifu,huruma na heshima kwa wazazi,majirani pamoja na viongozi kuendeleza umoja na mshikamano katika jamii.

“Mwanamke nakuomba uinuke angalia nafasi yako ya malezi katika familia yako inasimama wapi,tumetembelea Wilaya zote za mkoa wa Kagera na kubaini changamoto mbalimbalimbali zinazowakumba watoto wetu hasa wa kiume ambazo ni unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ulawiti na ubakaji”amesema 

Amesema changamoto zinazowakumba watoto wa kiume si ya kawaida kama jamii inavyoichukulia maana wazazi wanaichukulia katika hari ya kawaida lakini changamoto hiyo ilivyokubwa itasabaisha miaka ya mbele kukosa wanaume watakaokuja kuwaoa mabinti wajao.

Pia amewashauri wazazi kupita katika shule na kutafuta tarifa za watoto wao na kujua changamoto walizonazo ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na kuzifanyia kazi kabla hazijaleta madhala makubwa kuliko kuwaachia walimu peke yao hawawezi maana hili janga linahitaji nguvu ya kila mtu kwa nafasi yake”

Anato mfano kuwa mtoto ananza darasa la kwanza mpaka anamalzia darasa la saba mzazi hajawahi kukanyaga shuleni kwa sababu hajawahi kuitwa lakini angefika na kuonana na walimu pengine wangeweza kumueleza changamoto inayomkabili mtoto wake,pia wapo watu ambao tunawathamni na kuwaamini lakini hao ndio wanatumika katika kuharibu watoto wetu na tunakaa kimya eti kuficha aibu.

“Nawaomba wazazi wa kike tupaze sauti tunapowaona wanaume wanawalawiti watoto wetu ili wachukuliwe hatua kali za kisheria kwani sisi ndiyo tunaopata hasara baba akimlawiti mtoto akaondoka hasara inabaki kwako maana huyo si wa kiume tena bali atabaki kama mdada wa nyumbani akiamaka anafagia uwanja na kuosha vyombo hana kazi nyingine tuone uchungu maana watoto wanaofanyiwa haya tunao majumbani  na majirani zetu tunabaki kusema mtoto wa fulani kwa kesho anawezakumuambukiza wa kwako”ameeleza 

"Katika zama hizi ambapo watu hususani vijana wanakabiliwa na changamoto za kimaadili ni wajibu wetu kama waislam kuenzi mafunzo ya kidini na kuyatumia katika maisha ya kila siku kwani watu wakiishi bila  maadili bora kwenye jamii haiwezi kuendelea,kuwa na Amani,haki,kusisitiza juu ya tabia njema na uongozi bora"ameeleza

Mwendesha mashitaka Ajuaye Bilishanga  amesema kuwa zipokauli kuwa wanawake wanajisahau katika malezi ya watoto wanajisahau sana katika malezi na kutumia muda mwingi katika kutafuta maisha matokeo yake hawajui watoto wao wanakua katika misingi ipi akijakushutuka mtoto anakuwa ameishaharibika.

“wazazi wameacha watoto wajilee,hawajishughulishi na malezi yao na hawagundui mabadiliko waliyonayo watoto wao ndiyo maana unakuta wanalawitiwa na kubakwa lakini imegundulika kwamba wengi wanalawitiwa na wazazi wao hawajui kabisa mpaka mtoto anapopatwa na madhara mfano kushindwa kutembea,mtoto amepatwa ujauzito,magonjwa makubwa kule mahakamani tunakutana na watoto na wakiishachelewa kutoa taarifa za kesi nyingi zinaharibika”

Amesema hari hiyo inawasababishia wazazi waonekana kuna sehemu hawafanyi vizuri katika malezi ya watoto wao hivyo, akina mama wana wajibu ambao mwenyezi Mungu amewapatia na siku ya mwisho utawaulizwa alikupatia watoto je uliwalea vipi?

Kwa upande wa mratibu wa dawati la jinsia na watoto  Polisi Wilaya ya Bukoba Petrida Minga  amewataka watoto kutoa taarifa wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji hususani ubakaji na ulawiti kwani wasipofanya hivyo wanahatarisha Afya zao, ikiwemo kifo hivyo usimuonee aibu wala huruma mtu anayefanya hivyo kwani hana nia njema na maisha yako.

“Watoto wengi wanaingiliwa kwa sababu zifuatazo ya kwanza wazazi wanachangia kwani wapo wazazi wanaowatumia watoto wao kama vitega uchumi,wapo wanaodiliki kuwaambia watoto wao kwamba umeishakuwa mtu mzima nawewe utafute"ameeleza Petrida

 Amesema wanakutana na kesi kama hizo sana mfano mtoto analazimishwa kwenda kufanya biashara katika maeneo hatarishi usiku hasa kwenye baa na ajiuze mwili wake.

Pia jingine watoto wakibakwa au kulawitiwa mzazi anapokea milioni mbili anamwambia mtoto asiende kutoa ushahidi pale kesi inapofunguliwa mzazi anaona fedha inathamani zaidi ya maisha ya mtoto wake hivyo,hii inapleekea kushindwa kesi  mahakamani hari inayowaachia makovu na simanzi watoto hao waliotendewa maovu.










Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top