Rais Dkt. Samia Azindua Kituo Cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC)

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (EACLC), ambacho hadi sasa kimetumia zaidi ya Shilingi bilioni 282.7. Mradi huo mkubwa umejumuisha ujenzi wa jumla ya maeneo 2,060 kwa ajili ya maduka na ofisi, na unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 15,000 za moja kwa moja na takribani ajira zisizo rasmi 50,000.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Samia amepongeza EACLC kwa kutekeleza mradi huo wa kimkakati na kusema kuwa Kituo hiki hakikuanzishwa kwa lengo la kushindana na Soko la Kariakoo, bali kuwa mfano bora wa kisasa wa namna biashara inavyoweza kuendeshwa kwa ufanisi zaidi. Amesisitiza kuwa Kariakoo kinaweza kujifunza kutoka EACLC, hasa katika matumizi ya teknolojia ya kisasa na mbinu za kuzuia upotevu wa mapato ya serikali.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top