MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Kyerwa mkoani Kagera Khaldi Mussa Nsekela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechukua na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo katika ofisi za tume huru ya uchaguzi leo.
Baada ya kurejesha fomu hiyo Nsekela ameongea na wananchi na wanachama wa wa CCM ambapo amewaeleza kuwa muda wa kampeni ukifika atapita kila kitongoji,kijiji na kata ili kutafuta kura za chama hicho ambapo amewashauri wananchi wa Kyerwa kujitokeza kupiga kura ufikapo Oktoba 29 ili kuchagua viongozi watakao waongoza na kuwaletea amendeleo ya kweli kupitia CCM.