NEMC Yashiriki Kikao Cha Wadau Kuhusu Usimamizi wa Taka za Kielekroniki

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lashiriki kikao cha wadau kuhusu usimamizi wa taka za kielektroniki kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WEEE Centre Tanzania kujadili fursa, changamoto na mikakati ya usimamizi endelevu wa taka za kielektroniki nchini.

Kikao hicho kilifanyika Dodoma na kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali zikiwemo TCRA, TBS, TIRDO, UDSM, COSTECH, PPP, e-GA, TAMISEMI, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Tume ya TEHAMA, TARA, CTI na kampuni ya Chilambo General Traders Ltd.

NEMC ilipata fursa ya kuendelea kuelimisha wadau kuhusu umuhimu wa kusimamia aina hii ya taka hatarishi (e-waste) kwani athari zake zinachukua muda mrefu kutokea. Pamoja na uwepo wa sera, sheria na kanuni zinazoelekeza usimamizi wa taka za kielektroniki, uelewa bado haujafikia wadau wote. Maazimio ya kikao yakaelekeza kujenga uelewa pamoja na kuimarisha ushirikiano wa taasisi na jamii ili kuwa na usimamizi endelevu wa taka za kielektroniki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top