Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekutana na kufanya mazungumzo na Taasisi ya ASEZ (Save the Earth from A to Z) kwa lengo la kujadilana na kupanga mikakati inayohusu masuala ya Usimamizi na uhifadhi wa Mazingira.
Katika Kikao hicho Taasisi ya ASEZ imeainisha majukumu yake kuwa ni kujishughulisha na masuala ya Uhifadhi wa Mazingira, Udhibiti wa uhalifu, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya utunzaji wa Mazingira na mashirikiano na wadau mbalimbali katika Utekelezaji wa kufikia malengo ya Dunia yenye amani "𝐇𝐚𝐩𝐩𝐲 𝐅𝐮𝐭𝐮𝐫𝐞"
Baraza linaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutekeleza Sheria ya Usimamizi wa Mazingira nchini kwa mustakabali wa Mazingira safi, salama na kwa maendeleo endelevu ya Taifa.