Khalid Nsekela Ateuliwa Kugombea Ubunge Jimbo la Kyerwa

0


Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kyerwa mkoani Kagera,Mwalimu Ramadhan Marwa amemteua mgombea wa chama cha Mapinduzi (CCM) Khalid Mussa Nsekela kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Mwalimu Marwa ametangaza uteuzi huo mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchambuzi na uhakiki wa wagombea walioonesha nia ya kuwania nafasi hiyo.

Marwa amesema Nsekela ametimiza vigezo vyote vinavyotakiwa kikatiba,  kisheria,kikanuni na kuwasilishaji nyaraka sahihi.

Nsekela mwenye shahada ya uzamili katika usimamizi wa biashara na masoko ya kimataifa na shahada ya uzamili ya dipromasi ya uchumi katika mahojiano mafupi baada ya uteuzi huo, ameahidi kufanya kampeni za kistaarabu,kudumisha amani,upendo na kuzingatia hoja na masuala ya msingi yatakayomuongoza kutatua changamoto zinazowakabili  wakazi wa Kyerwa.

Pia ametoa shukrani kwa CCM kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa na wananchi wote wa Kyerwa bila kujali itikadi zao za vyama kwa ushirikiano ambao wanaendelea kumpatia na imani ambayo wamemkopesha hivyo, akwaomba washiriki kufanya kampeni za kistaarabu na amani ili ifikapo Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo ya kweli kupitia CCM.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top