Je Tanesco Wanatoa Fidia Kiasi Gani Kwa Mtu Aliyepoteza Maisha Kutokana na Umeme?

0


#Elimu: Katika maeneo mengi ya mijini na vijijini, bado kuna uelewa mdogo kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa nishati ya umeme. 

Katika maeneo hayo swali ambalo huulizwa mara kwa mara na wakazi wa maeneo mbalimbali ni: “Je, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hutoa fidia kwa mtu aliyefariki dunia kutokana na ajali ya umeme?

Hili limekuwa ni swali linaloibuka hasa pale kunapojitokeza matukio  yanayosababishwa na hitilafu ya umeme.

Kwa mujibu wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) ni kwamba;

TANESCO hawatoi fidia kwa mtu ambaye ni Marehemu. Kwa mujibu wa kanuni ya 23(1) na (2) ya Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Upelekaji, na Usambazaji Umeme za Mwaka 2023 imeeleza kuwa, anayeweza kufidiwa ni mtu aliyeumia au kupoteza Mali zake.

✍️Imeandikwa na Emmanuel Chibasa

Chanzo: ewura ccc

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top