#UKATAJI WA MAJI
Kanuni za ubora wa huduma za Maji na Usafi wa Mazingira( Ubora wa Huduma na Leseni za Mwaka 2020; Tangazo la serikali Na: 849, Viwango vya ubora wa huduma pamoja na gharama za fidia kwa kushindwa kufikia viwango vilivyowekwa. Kanuni ya 34(3) inazitaka mamlaka za maji zilizopewa leseni kufikia viwango vya kutoa huduma zitakazowajibika kulipa fidia kwa waathirika.
Kanuni za ubora wa huduma za maji na usafi wa Mazingira inaeleza kuwa endapo mteja amekatiwa huduma ya maji kimakosa itatakiwa ndani ya masaa 24 huduma kurejeshwa baada ya taarifa kutolewa na endapo mtoa huduma atashindwa kufikia viwango vilivyowekwa mtoa huduma atamlipa mteja shilingi 100,000.00 fidia ya msingi na shilingi 5,000 kwa kila siku inayoongezeka bila tatizo kutatuliwa.
Imeandikwa na Emmanuel Chibasa
Chanzo: ewura ccc