Wanufaika wa Mikopo ya Asilimia 10 Tabora Watakiwa Kutumia Teknolojia Kupata Masoko

0


MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Sauda Mtondoo amewataka Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu waliokopeshwa sh. 401.1 milioni  kuwa wapekuzi na kutumia teknolojia ya simu janja kufanya Biashara Mtandao.

Sauda ametoa wito huo wakati wa hafla fupi ya kutoa mikopo kwa vikundi 11 vya vijana, vikundi 17 vya wanawake na vikundi vitatu vya watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Maxweli mjini hapa.

‘’Simu yako isiwe ya kujipiga selfii na kutuma Istagram na Facebook tu, unaweza kuwa Igunga lakini unafanya biashara na watu waliopo nje ya Igunga na unaweza kupokea biashara kutoka Mwanza au Dar es Salaam,’’ amesema. 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Hiyo, Selwa Hamid amempongeza na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha mikopo hiyo ambayo inamgusa mtu mmoja mmoja. 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top