Serikali Yaboresha Mazingira ya Kujifunzia Kwa Wenye Ulemavu-Profesa Mkenda

0


Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewaagiza wamiliki wa shule nchini kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa watoto wote hasa wale wenye ulemavu ili kuhakikisha makundi yote yanafikiwa na elimu jumuishi.

Waziri Mkenda ameyabainisha hayo Jijini Mwanza kwenye mkutano wa Wanawake Wamiliki wa Shule binafsi nchini kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vya kati na kuongeza kuwa jitihada zinazofanywa na Serikali zakuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na fursa ya elimu, ni vyema sekta binafsi nao waongeze kasi yakuleta mageuzi ya elimu.

Aidha ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ili wahitimu wanapokwenda mtaani wasikose ajira hata zile za kujiajiri wenyewe.

Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amefafanua kuhusu tozo mbalimbali za vifaa vya elimu zinazotolewa huku akiwaahidi wamiliki hao kukutana nao nakujadiliana . 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewashauri wamiliki wa shule binafsi na vyuo kuiunga mkono serikali kwa vitendo ili kuhakikisha taifa linapata maendeleo kupitia sekta ya Elimu.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top