Idadi ya Utumiaji wa Huduma ya Inteneti Nchini Yaongezeka Kwa Asilimia 9.6

0


 Huduma ya intaneti inaonesha kuongezeka utumiaji kutoka milioni 49.3 mwezi Machi 2025 hadi kufikia milioni 54.1 mwezi Juni 2025 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 9.6.

Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano ya robo mwaka inayoishia Juni 2025 inaonesha idadi ya utumiaji wa intaneti inatokana na laini/waya ambazo zimetumia huduma ya Intaneti angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bila kujali teknolojia iliyotumika (FTTX, 2G - GPRS na EDGE, 3G, 4G, au 5G).

Ripoti hiyo imefafanua kuwa huduma ya intaneti kwa njia ya simu ya mkononi inapendelewa zaidi (99.5%) ikilinganishwa na huduma ya intaneti isiyohashimishika. 

Kuongezeka kwa utumiaji wa intaneti unatokana na ubora wa huduma na miundombinu inayowezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi.

Tembelea tovuti ya TCRA (www.tcra.go.tz), au kupitia kiunganisho https://bit.ly/44tXbii ilikupitia ripoti kamili ya sekta ya mawasiliano (Aprili - Juni 2025).

Chanzo: tcratz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top