Dkt. Ntuli Awataka Wadau wa Lishe Kuendelea Kuunga Mkono Jitihada za Serikali Kuimarisha Hali ya Lishe Nchini.

0


Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC), Dkt. Ntuli Kapologwe, amewataka wadau kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha hali ya lishe nchini. Dkt. Kapologwe ametoa rai hiyo wakati akifungua mkutano wa 39 wa Jukwaa la Wadau wa Uongezaji Virutubushi kwenye Vyakula Tanzania (TFFA) unaofanyika jijini Arusha.

Dkt. Kapologwe amesema kuwa ECSA-HC itaendelea kushirikiana na TFFA ikiwa ni kuunga mkono jitihada za jukwaa hilo pamoja na Serikali katika utekelezaji wa afua mbalimbali za kilishe hususani kwenye suala la uongezaji wa viritubishi kwenye vyakula.

 “ili kuipa lishe kipaumbele mnaweza kuona hata sisi katika mpango mkakati wetu wa miaka 10, lishe ni moja ya malengo tisa yaliyoingizwa katika mpango mkakati wetu, lengo likiwa kushiriki kikamilifu  katika utekelezaji wa afua za lishe nchini” Amesema Dkt. Kapologwe.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa TFFA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la SANKU Bw. Gwao Omari Gwao, amesema Jukwaa hilo limekutana kwa mara ya 39 tangu kuanzishwa kwake, lengo kubwa likiwa kuwakutanisha wadau na kujadiliana changamoto mbalimbali katika eneo la urutubishaji.

“Jukwaa hili linatukutanisha wadau mbalimbali pamoja na Serikali, ambapo kupitia mkutano huu tutaweza kutengeneza mpango mkakati wa pamoja wa miezi sita, ambao utaeleza maeneo ya kimkakati tunayotarajia kuyatekeleza kwa pamoja” Amesema Gwao.

Mkutano huo wa 39 wa Jukwaa la Wadau wa Uongezaji Virutubishi kwenye Vyakula nchini Tanzania (TFFA) utafanyika kwa muda Siku mbili jijini Arusha na umewakutanisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya urutubishaji wa vyakula wakiwemo kutoka Wizarani, Taasisi za Serikali, Vyuo Vikuu, Mashirika ya  Maendeleo na wadau wengine.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top