Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Taasisi ya Benjamin Mkapa wameingia makubaliano ya ushirikiano wa pamoja kwa kuimarisha na kukuza uwekezaji katika sekta ya afya nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri, amesema kuwa BMF imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya na kuongeza kuwa ushirikiano huu utaongeza mvuto kwa wawekezaji kwenye sekta hiyo muhimu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa BMF, Dkt. Ellen Mkondya Senkoro, alisema kuwa wamekuwa wakifanya juhudi za kutafuta wawekezaji katika sekta ya afya, na kupitia ushirikiano huu na TIC, wana matumaini kuwa utazaa matokeo chanya katika juhudi za kuhamasisha na kuwezesha uwekezaji katika sekta ya afya nchini.
Makubaliano hayo yalishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Dkt. Binilith Mahenge.