Tarura Wapongezwa na Serikali

0


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa amebainisha kuwa Serikali inatambua jitihada na kazi nzuri inayofanywa na Wakala  ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), akimsihi Mtendaji Mkuu Mhandisi Victor Seff na wasaidizi wake kutokatishwa tamaa na baadhi ya watu wa mitandaoni.

Waziri Mchengerwa ameeleza kwamba Wizara yake, Serikali na Bunge la Tanzania wanatambua kazi nzuri inayofanywa na TARURA katika kutekeleza maagizo, maelekezo na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema  kuwa Serikali pia inatambua ukubwa wa mahitaji hivyo kuwataka waendelee kuchapa kazi ili kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na kuwafungulia wananchi uchumi.

"Nipongeze jitihada na kazi kubwa inayofanywa na TARURA kuanzia kwa Mtendaji Mkuu wa TARURA na timu yako, ninawaamini sana, fanyeni kazi wala msirudi nyuma hata kidogo”.

“Bunge na hata wananchi wanajua kazi yenu kwahiyo msikate tamaa, msikatishwe tamaa na yeyote na wale wanaoandika andika huko, kazi yenu sisi Serikali tunaijua, endeleeni kufanya  kazi, Taifa letu ni Taifa changa na kila eneo kuna uhitaji, lakini Taifa letu pia ni kubwa na kila sehemu kuna uhitaji", amesema Waziri Mchengerwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top