Tanzania na Norway Kushirikiana Kwenye Mradi wa Nishati

0


Tanzania kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yafanya mashirikiano na Nchi ya Norway kwenye eneo la Nishati kupitia Mradi wa Energy for Development (EfD) kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya Norway (Norwegian Environment Agency - NEA).

Mradi huu ambao utatekelezwa nchini Tanzania, Msumbiji na Nigeria unalenga kukuza matumizi ya nishati jadidifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hasa katika kupunguza umasikini kupitia upatikanaji wa nishati bora.

NEMC na NEA wamekubaliana kushirikiana katika utekelezaji wa mradi huo ambao utasaidia kujenga uwezo wa kitaasisi kwa kuboresha kanuni na miongozo ya kimazingira, kutoa mafunzo kwa watumishi na kuimarisha uwezo wa kufuatilia ubora wa hewa, hususan katika miradi ya sekta ya mafuta na gesi asilia.

#Nemc

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top