Rais Mwinyi Awakaribisha Wawekezaji Kutoka China

0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha Wawekezaji kutoka China kuwekeza nchini hususan kuendeleza sekta   Ya afya na tafiti za dawa za asili nchini. 

Rias Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Timu ya  Wataalamu  kutoka Chuo cha Utafiti wa  Dawa za Asili cha China waliofika Ikulu kuonana naye.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi  amesema Zanzibar  imeendelea kuthamini  mchango na misaada ya China kwa Zanzibar katika sekta tofauti  za  Maendeleo na Kijamii  iliyodumu kwa muda mrefu tangu na baada ya Mapinduzi na kuendelea hadi sasa.   

Halikadhalika, ameeleza kufarijika na misaada katika Sekta ya Afya inayotolewa na timu za Madaktari Bingwa wanaokuja nchini kwa nyakati tofauti kutoa matibabu kwa Jamii, Dawa na huduma katika Hospitali na vituo vya afya na mafunzo kwa watendaji wa Sekta ya Afyanchini.

Naye Kiongozi  wa Ujumbe huo Naibu Mkurugenzi wa Chuo cha Utafiti wa Dawa za Asili cha  China Professa  Song Li Jwan amesema Ziara yao Zanzibar imelenga kuimarisha ushirikiano baina ya China na Zanzibar hususan katika  Maendeleo ya Sekta ya Afya na kuendeleza Tafiti za dawa za Asili  baina ya pande hizo mbili. 

 Amebainisha kuwa  hatua hiyo ni Utekelezaji wa Sera ya kitaifa ya China kwa Nchi za Afrika ikiwa ni utekelezaji wa  Malengo ya Mkutano wa Beijing  wa mwaka 2024  uliojikita katika Uimarishaji wa Sekta ya Afya.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top