NEMC Yawajengea Uwezo Wawekezaji Temeke Juu ya Masuala ya Uzingatiaji wa Sheria

0


Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Temeke Juni 18, 2025 limeendesha warsha ya kujengeana uwezo kwa Wawekezaji wenye Viwanda katika Wilaya ya Temeke kuhusiana na masuala mbalimbali ya Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Akizungumza, Meneja wa Kanda ya Temeke (NEMC) Bw. Abeli Sembeka wakati akitoa wasilisho kuhusu ufanyaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira amesisitiza wawekezaji kutekeleza masharti yanayowekwa kwenye cheti mara baada ya kukamilika kwa mchakato huo kwani kumekuwa na changamoto kwa wawekezaji wengi kutofanya yale yanayopaswa kufanyika kwa mujibu wa maelekezo ya cheti cha Mazingira.

Naye Meneja wa Uzingatiaji wa Sheria Bw. Hamadi Taimuru amewataka  wawekezaji hao kuwa mabalozi kwa wengine.

“Tunatarajia wadau hawa kwenda kuwa mabalozi wazuri wa masuala ya uzingatiaji wa Sheria kwa wadau wengine kutokana na elimu tuliowapatia leo” Amesema Bw. Taimuru.

Akiongea kwa niaba ya wawekezaji waliojitokeza,  Afisa wa Maabara za Zenufa (Zenufa Laboratories Limited) Bi. Fatma Shabani ameishukuru NEMC kwa kuandaa washa ya  utoaji elimu kwa wamiliki wa viwanda na ametoa rai kwa Baraza kuendelea na utaratibu huo wa kutoa elimu kwa wawekezaji ili Mazingira yaendelee kutunzwa.

Wadau wengine walioshiriki katika warsha hiyo ni Maafisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Temeke na Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda Tanzania.













Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top