NEMC Yapongezwa Kwa Kuendelea Kusimama Sheria ya Usimamizi wa Mazingira

0


Mkuu wa Wilaya Ubungo Mhe. Albert Msando amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kuendelea kusimamia Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.

Mhe. Albert Msando ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la NEMC katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa ngazi ya Mkoa yaliyofanyika leo 14 Juni, 2025 katika viwanja vya Makuburi Jijini Dar es Salaam.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila katika nafasi ya mgeni rasmi, Mhe. Msando ameitaka NEMC kuwekeza nguvu zaidi katika udhibiti wa kelele chafuzi za viwadani kwani zinakuwa kero kubwa kwa baadhi ya wakazi wanaoishi karibu na viwanda hivyo na pia kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya udhibiti wa taka ngumu ili zisizagae kwenye Mazingira na kusababisha uchafuzi wa Mazingira.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabada ya wadau mbalimbali walioshiriki Maadhimisho hayo Mhe. Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa Viongozi wa mamlaka mbalimbali zikiwemo Serikali za mitaa kuendelea kutoa elimu kwa umma juu udhibiti wa taka, kushirikiana kudhibiti  matumizi ya mifuko ya  plastiki ambapo pia emeitaka jamii kuepuka shughuli zozote zinazoharibu Mazingira, kuepuka Uchimbaji mchanga holela na upanuzi wa miji usiozingatia mipango miji.

Aidha Maadhimisho hayo yaliambatana na ugawaji wa tuzo na zawadi kwa wadau mbalimbali walioibuka kinara katika shughuli za utunzaji na uhifadhi wa Mazingira.

Maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na taasisi na wadau mbalimbali wa Mazingira yaliambatana na Kauli mbiu isemayo "Mazingira yetu na Tanzania ijayo tuwajibike sasa; Dhibiti matumizi ya plastiki" ambayo pia ni Kaulimbiu ya Siku ya Mazingira Duniani kwa mwaka 2025 iliyoadhimishwa Juni 5 Mwaka huu.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top