Nemc, Osha na Halmashauri Zatakiwa Kuwasimamia Wachimbaji Wadogo

0



Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC), Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) na Halmashauri za Mji zatakiwa kuwasimamia na kuwaelekeza wachimbaji wadogo wa madini namna  bora ya kuchimba madini bila kuharibu mifumo yoyote ya mazingira pamoja na kuzingatia Usalama wa Afya mahali Pa kazi wakati wa shughuli za uchimbaji madini zinafanyika.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa  wakati anafunga maonesho ya madini na fursa za uwekezaji wilayani Ruagwa kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Dkt. Kiruswa alisema kuwa, Serikali inazipongeza taasisi zote zilitoa mafunzo mbalimbali wakati wa maonesho kwa wachimbaji wadogo wa madini yaliyohusu namna ya  bora uchimbaji na uchenjuaji madini kwa kufuata mifumo ya kitaalamu pamoja maendeleo  ya Sayansi na teknolojia.

Dkt.Kiruswa aliongeza kuwa,  Serikali itaendelea kutoa leseni kwa wachimbaji wadogo katika maeneo mbalimbali  yaliyofanyiwa utafiti wa jiosayansi ili kuwasaidia wachimbaji wadogo kufanya uchimbaji katika maeneo yenye tija bila kupoteza mitaji kama Vision 2030 inavyosema, Madini ni Maisha na Utajiri.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alisema kuwa, Mkoa wa Lindi utaendelea kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Madini ili kuongeza uwekezaji unaofungamanisha  Sekta ya Madini na Sekta  nyingine za kiuchumi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa Lindi  na mikoa jirani inayopakana na Lindi.

Naye, Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Lindi Mayunga Mussa aliipongeza Wizara ya Madini kwa kazi nzuri inayofanya hususan katika kusimamia na kuendeleza Sekta ya Madini ambapo katika  kipindi cha mwaka 2019 hadi 2020 makusanyo ya maduhuli kwenye Sekta ya Madini yalikuwa shilingi bilioni 1.5 mkoani Lindi ila sasa yameongezeka mpaka kufikia shilingi bilioni 8.1 kwa mwaka 2024/2025.

Maonesho hayo yalifanyika kwa  Kaulimbiu inayosema "Madini na Uwekezaji Fursa za Kiuchumi Lindi , Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top